Psalms 21

Shukrani Kwa Mungu Kwa Ajili Ya Ushindi

(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi)


1 aEe Bwana, mfalme huzifurahia nguvu zako.
Tazama jinsi ilivyo kuu furaha yake
kwa ushindi unaompa!

2 bUmempa haja ya moyo wake
na hukumzuilia maombi ya midomo yake.

3 cUlimkaribisha kwa baraka tele
na kumvika taji ya dhahabu safi kichwani pake.

4 dAlikuomba maisha, nawe ukampa,
wingi wa siku milele na milele.

5 eKutokana na ushindi uliompa, utukufu wake ni mkubwa,
umeweka juu yake fahari na utukufu.

6 fHakika umempa baraka za milele,
umemfanya awe na furaha
kwa shangwe ya uwepo wako.

7 gKwa kuwa mfalme anamtumaini Bwana;
kwa upendo usiokoma wa Aliye Juu Sana hatatikiswa.


8 hMkono wako utawashika adui zako wote,
mkono wako wa kuume utawakamata adui zako.

9 iWakati utakapojitokeza
utawafanya kama tanuru ya moto.
Katika ghadhabu yake Bwana atawameza,
moto wake utawateketeza.

10 jUtawaangamiza wazao wao kutoka duniani,
uzao wao kutoka wanadamu.

11 kIngawa watapanga mabaya dhidi yako
na kutunga hila, hawawezi kufanikiwa,

12 lkwa kuwa utawafanya wakimbie
utakapowalenga usoni pao
kwa mshale kutoka kwenye upinde wako.


13 mEe Bwana, utukuzwe katika nguvu zako,
tutaimba na kusifu nguvu zako.
Copyright information for SwhKC